Mara ngapi umesikia wazazi wa Kimarekani wanaolilia watoto wao waliopelekwa na Joji 'Kichaka' huko Iraq wakiwa hawana matumaini ya kurejea tena?
Mara ngapi umesikia kuhusu kilichotokea Rwanda, na sasa kinatokea tena Dafur na halafu wote tukajifanya kutokuwa na habari?
Mara ngapi umesikia kuhusu Robert Mugabe akiua watu wake kwa kisingizio cha kuwakomesha 'mabwana' wakubwa wa Magharibi?
Mara ngapi umesikia mwanasiasa wako akikupa ahadi za maisha matamu, kisha akajituniku mwenyewe?
Tazama,
Kungali na giza totoro sitakoma kuingoja nuru
Mjumbe atarejea tena.
Tumaini litarejea tena.
3 comments:
Maneno poa lakini tumaini litarejea tena kivipi?
Kaka Mwandani, Ukitazama kwa makini duniani yetu imekuwa katika giza totoro kwa muda wa miaka kama minane hivi, watu wamepoteza matumaini kabisa. Joji Kichaka na Osama kwa kiasi kikubwa wamechangi sana kwa kutoweka kwa tumaini hilo.
Lakini ukitazama picha yangu utagundua kuwa pamoja na unyama unaoendelea kila siku katika dunia hii, jua haliachi kuchomoza kila kukicha na ndege hawaachi kuruka tena. Hii ni ishara kuwa penye giza mwanga utaangaza tena na ndege wataimba tena, TUMAINI LITAREJEA TENA!
Bush, Osama, Mugabe, kama ilivyokuwa kwa Saddam, wamekuja na watapita na Amani itakuwako tena. Ni swala la muda tu. TUMAINI LITAREJEA TENA!
ni kweli eti maisha bora kwa kila mtu halafu anajipa yeye na familia yake kwanza.Unajua wanasiasa ndio walioifikisha dunia hii yetu hapa tulipo kwa bahati mbaya zaidi ndio wanaoongoza hii dunia
DAUDI AMIRI MMBAGA
Post a Comment