Wednesday, June 6, 2007

MISAADA YA WLIOENDELEA NI UPPUZI KWA MWAFRIKA

Huyu ni Andrew Mwenda, mwandishi wa habari na mtaalamu wa masuala ya jamii toka Uganda.
Jamaa ana mzuka balaa. Anawashambulia wazungu wanaoleta misaada kwa waafrika bila kufanya tathmini kuwa misaada hiyo inamsaidia nani.

Ayayayayaya! Jamaa anaenda mbele zaidi na kuzipiga shuti serikali za kiafrika kuwa hazijafanya chochote kwa kupitia misaada. Anasema misaada inawalemaza waafrika.
Anaiuliza hadhira sasa iwapo kuna yoyote anayefahamu nchi iliyoendelea kwa kupewa misaada. Watu kimyaaaaa! Halafu ghafla kuna mtu ananyoosha mkono, uliza ni nani? Bono, yule mwanamuziki maarufu wa Rock ambaye amevalia njuga kwelikweli vita dhidi ya umasikini Afrika. Yuko hapa, alitakiwa awe kwenye mkutano wa G8 ila amewatoroka.

Bono anapatiwa nafasi ya kuongea na kuitolea mfano nchi yake ya uzaliwa, Northern Ireland kuwa ni nchi mmoja wapo amabyo imetumia misaada kuisimama kwa miguu yake mwenyewe.

Wanabishana na mwenda lakini baada ya mkutano wanakaa pamoja na kupata mvinyo. Wanakubaliana kutokubaliana. Kula leki TED!

3 comments:

Anonymous said...

Bono amekosea. Nchi yake, Republic of Ireland (siyo Northern Ireland) imeendelea sana kwa miaka ishirini sasa. Lakini siyo k.s. ya msaada (Ireland imepokea msaada kutoka Umoja ya Ulaya au EU). Kuna studies nyingi ambazo wanatuambia hivyo.

Northern Ireland inapokea msaada kubwa kutoka London and EU pia, lakini bado uchumi yake uko hoi k.s. ya vita ya miaka 30.

Bono ni mwimbaji, siyo mwanauchumi...

Peter (DSM)

Anonymous said...

Ndio bwana Peter nakubaliana na wewe kabisa, ila nadhani pia kuwa unaelewa kuwa katika dunia ya leo ya teknolojia na utandawazi hakuna ukweli mmoja.

Kwa jinsi jamaa hawa wawili walivyoziwakilisha mada zao kila mmoja alikuwa na hoja ya msingi ndio maana hata wakafikia hatua ya kukubaliana kutokubalina. Falsafa babkubwa sana hii.

Kwa habari za kina tafadhali msome Ethan Zuckerman wa www.ethanzuckerman.com

Anonymous said...

sawa ndugu. Sitaki kuwa 'post modern' sana, hata kwenye dunia ya jembe la kienyeji, hamna ukweli mmoja tu.

Mimi binafsi niliamua kutokubaliana na Mh. Bono zamani sana!

Nimeshatoa maoni yangu kwa blog ya EZ tayari. Lakini hamna mapya. Nililalamika kuhusa Mt. Bono tu, kama kawa. Nimefanya hivyo kwani ana jukwaa kubwa kwa maoni yake k.s. ya umaarufu wake, lakini mara nyingi ujuzi wake siyo kamili.