Tuesday, June 5, 2007

KARIBU KWA MWENYE MACHO...Karibu kwenye blogu ya Mwenye Macho... Blogu hii itakuwa ni ya picha zaidi kuliko maneno. Naitwa Babukadja Sankofa Msangi(ama kwa jina la zamani Philemon). Kwa bahati iliyo njema blogu hii inazaliwa siku moja baada ya kuanza kwa mkutano mkubwa wa maswala ya teknolojia, burudani na ubunifu yani TED. Nafurahi kukuletea habari za mkutano huu kwa njia ya picha. KARIBU!

7 comments:

ndesanjo said...

Haambiwi tazama...
Karibu sana. Nategemea tutaelimishwa na kuburudishwa na kazi zako.

Bob Sankofa said...

Ni kweli kabisa Ndesanjo. Blogu ni kama dawa ya kulevya, kabla hujaitilia maanani unaona haina thamani. Ila ukiianza bwana, kila ukipata kitu unataka ukikimbize mara moja. Yani kama teja kaonyeshwa unga. :-)

Mlioko nje mnachelewa, twendeni sasa.

Egidio Ndabagoye said...

Karibu Bob Sankofa.Sisemi sana natazama tu!

Bob Sankofa said...

Egidio asante sana kwa kuniunga mkono, wewe unayo blogu?

Bwaya said...

Karibu sana Sankofa!

Anonymous said...

Tutakuwa pamoja ndugu, mimi sina blogu ila nimsomaji mzuri wa blogu karibu zote hasa zenye mtazamo wa kiafrika- Mlewa(Amani ensemble)

kibongobongo said...

nawa mwenye macho nimekukubali, naomba tupeana updates kuhusu TED na ikiwezekana tuufungue uma zaidi kuhusu mkutano huu kwani hii ndio kazi yetu wanablogu(ingawa mimi ndio nimeingia kwenye fani kama http://www.mnyama.blogspot.com)

Namaanisha kuwafungua kwa mtindo wa kuwafanya wahudhurie kwa wingi zaidi na sio kwa kuwaelezea tu nini kilichojiri.

Ahsante.