Friday, June 8, 2007

TED IMEFIKA TAMATI

Mkutano uekwisha, ulikuwa murua. Hapa watu wameongeza marafiki, wameongeza anuani, wameongeza miradi ya kufanya mwaka huu.

www.mwenyemacho.blogspot.com imezaliwa pia na imepatiwa nyenzo ya kuifanya iwe bora zaidi, laptop (Mac Book Pro) ya bure toka Google. Pamoja na radio ya Satelite ambayo itaiwezesha Mwenye Macho kupata habari kadha wa kadha na kuzitupa kwenye blogu hii. Kaa mkao wa kula.

Wosia wangu kwa watanzania ni kuwa tujitahidi kuhudhuria semeina au workshop au mkutano japo mmoja kwa mwaka. Kwani huwezi kujua kuwa utakutana na nani na utafungua milango gani katika masha yako.

Nimesikitishwa na kitu kimoja, mkutano umefanyika Tanzania lakini waliopanda kutoa mada kwenye jukwaa la TED ni Watanzania wawili tu, Rais Kikwete na mjasiramali Ali Mufuruki.

Hata Watanzania waliohudhuria mkutano huu ni wa kuhesabu. Tujitahidi wakati mwingine na tuendelee kublogu kwa nguvu zote.

Naelekea nyumbani sasa. Nilikuja kwenye mkutano lakini nina kiporo niliacha. Natengeneza filamu iitwayo "Funguo" Itatoka muda sio mrefu. Endelea kufuatilia kurasa hizi ujue mustakabali wa mradi huu. Asante kwa kufuatili mkutano wa TED kupitia blogu hii na nyinginezo. Wakati mwingine...

6 comments:

Anonymous said...

Kazi murua Sankofa,
Twendeni tukalijenge taifa,tusije kuwa kama wale...

Anonymous said...

Jeff nakushukuru sana kwa kutembelea blogu hii changa. Tafadhali isambaze kwa wadau wengine huko ughaibuni

mwandani said...

Swafi sana. Umetuhabarisha vizuri... Ilikuwa kama niko hapo mkutanoni.

nakuomba usichoke, endelea kutuletea na mambo mengine mengi baada ya mkutano.

Christian Bwaya said...

Nimeipenda blogu yako kaka. Hongera kwa kazi nzuri ya kutuhabarisha yaliyojiri TED.

Afromusing said...

Nilifurahi kukutana nawe katika mkutano wa TED.

My swahili is defective as you may know, so i will revert back to my usual staple to say Thank you! It was great meeting you. Go Cheetahs!

Anonymous said...

Nawashukuruni sana kwa kutembelea blogu hii. Nitazidi kuhabarisha kila ninapopata kitu fulani.

PICHA MOJA HUZUNGUMZA MANENO ALFU MOJA!