Friday, June 15, 2007

KAZI NA DAWA

Hivi niliwahi kukuambia kuwa ninafanya kibarua na jamaa fulani wanajiita MEDIA FOR DEVELOPMENT INTERNATIONAL? Kama hapana basi hapo ndipo nilipo, na picha hii nimeipiga majira ya saa kumi kasorobo jioni ya leo. Nilivutiwa na jua lilikuwa linagonga hapo kwenye meza

Huyu aliyemo katika picha hii ni rafiki yangu anaitwa Paul Ndunguru au Baba Paka (Kwa ufafanuzi zaidi kuhusu hilo jina la pili muulize Ndesanjo Macha wa http://www.jikomboe.com/. Jamaa ni mchoraji wa katuni na mazagazaga mengine. Atakuwa na blogu hivi karibuni, umtembelee tafadhali. Hapa jamaa anapiga kazi huku anapata kababu na machicha ya nazi. Kazi na dawa bwana.


Picha hii pia niemiweka kwenye mtandao wa http://www.flickr.com/, tafadhali tembelea mtandao huu uone kazi za wapiga picha wengine. Huwa napata ideas nyingi sana humu.


Kuna kitu nimegundua baada ya kupiga picha hii, nadhani picha za Black and White bomba sana. Unaonaje nikiendelea kukuletea picha za mtindo huu hapa bloguni? Pale inapobidi tulete za rangi tutafanya hivyo. Naomba maoni

7 comments:

Anonymous said...

ndugu Mwenye Macho, mimi napenda sana black and white. Inaonyesha wazi umuhimu ya giza na ya mwanga pia.

Asante kwa taarifa zako kutoka kwa TED.

luihamu said...

Kaka badilisha TEMPLATE yako kisha weka picha za black and white la sivyo wengine hatuoni kabisa kama hii picha naona mwanga tu.

Nuff Nuff Respect.

mwandani said...

Naomba kufikisha salamu kwa Paul... mara ya mwisho New Delhi miaka ileee... sitasahau vichupa vya rangi ulivyoninunulia...sanaa idumu. Joe

Bob Sankofa said...

Kaka Kifimbocheza wewe pia unapiga Picha? Tafadhali tuzidi kushirikiana maujuzi.

Kaka Luihamu nafikiri inawezekana kuwa tarakilishi yako haikuwa na mwanga. Jaribu kuongeza brightness halafu punguza kidogo contrast.

Kaka Mwandani, kaka Paul amepokea salamu. Anasema hiyo siku mlikutana Delhi kuna jambo hukutaka kabisa kumuamini japo alikuapia kabisa. Sijui ilikuwa nini ila amefurahi sana pata salamu toka kwako.

Anonymous said...

Sankofa, mie siyo bwana picha! Takriban miaka 16 iloyopita, ilikuwa hobby yangu, lakini siku hizi sina hamu sana.

Nilipenda picha yako. Ulivutiwa na mwanga mezani. Na sisi tulivutiwa na picha.

Napendekeza picha zako ziwe kubwa zaidi kwenye blogu.

Pia, niliweka blog yako kwa 'blogroll' yangu. Kwa sababu sisi wawili tulianza hivi karibuni, pia nilipenda taarifa zako za TED.

Bob Sankofa said...

Nashukuru kwa kuweka kiunganishi cha blogu hii kwenye blogu yako, nami nitarejesha fadhila muda si mfupi.

Nashukuru pia kwa wazo la kukuza picha. Ila ukibofya hapo kwenye picha itakupeleka kwenye ukurasa amabo unakuapa ukubwa wa picha halishi.

Nina mpango wa kuanza kupandisha na video pia muda si mfupi.

Bob Sankofa said...

Nashukuru kwa kuweka kiunganishi cha blogu hii kwenye blogu yako, nami nitarejesha fadhila muda si mfupi.

Nashukuru pia kwa wazo la kukuza picha. Ila ukibofya hapo kwenye picha itakupeleka kwenye ukurasa amabo unakuapa ukubwa wa picha halishi.

Nina mpango wa kuanza kupandisha na video pia muda si mfupi.